Heri kwa Pasaka 2014

Wapendwa wasomaji wa Wazo huru,

Studio za Wazo huru na washirika wake tunapenda kuwatakieni Pasaka njema nyote. Alleluia , Kristo amefufuka. Amina.

Aidha, leo Wazo huru latimiza mwaka mmoja tangu lizaliwe Pasaka iliyopita

Hapa ni kwa kujikumbusha machache kuhusu tukio la ufufuko:

http://www.youtube.com/watch?v=P98Yq3xBRKc

http://www.youtube.com/watch?v=ygQhnqSn3TA

http://www.youtube.com/watch?v=Fq3lgmn_vMo

Matukio Katika Picha – Maaskofu wa Tanzania na Watanzania waishio Roma

Hivi punde tumekuwa tukizifuatilia habari za tukio la maaskofu wa Tanzania wakiwa katika Ad Limina huko Roma. Katika nyakati mbalimbali  baadhi ya maaskofu waliweza kupata wasaa wa kujumuika na watanzania waishio Roma ama kwa ibada ama kwa mijumuisho ya kawaida. Hapa  kuna baadhi tu ya picha zinazoashiria matukio hayo. Kwa wale ambao hawakubahatika kuzipata basi Wazo huru imefanikiwa kuzidaka hizo na kukurushia.

Gonga katika kiungo  kifuatacho:

https://www.dropbox.com/sh/9qeunwnc6y3vrz6/eCYeql5q8R

Mkutano wa Papa na Maaskofu wa Tanzania

Katika mkutano huo maarufu kama Ad Limina papa alifanikiwa kukutana na viongozi mbali mbali wa Kanisa wakiwemo Maaskofu toka Tanzania.

AUDIENCES

Vatican City, 7 April 2014 (VIS) – This morning, the Holy Father received in audience:

– Cardinal Fernando Filoni, prefect of the Congregation for the Evangelisation of Peoples.

– Archbishop Francis Assisi Chullikatt, J.C.D., permanent observer at the United Nations in New York and at the Organisation of American States.

– Ten prelates of the Tanzania Episcopal Conference, on their “ad limina” visit:

– Archbishop Jude Thaddeus Ruwa’ichi, O.F.M. Cap., of Mwanza, apostolic administrator of Shinyanga;

– Bishop Renatus Leonard Nkwande of Bunda;

– Bishop Damian Denis Dallu of Geita;

– Bishop Almachius Vincent Rweyongeza of Kayanga;

– Bishop Michael George Mabuga Msonganzila of Musoma;

– Bishop Severine Niwemugizi of Rulenge-Ngara;

– Archbishop Josaphat Louis Lebulu of Arusha;

– Bishop Beatus Kinyaiya, O.F.M. Cap., of Mbulu;

– Bishop Isaac Amani Massawe of Moshi;

– Bishop Rogath Fundimoya Kimaryo of Same.

This afternoon, he is scheduled to receive in audience His Majesty Abdullah II Ibn Al Hussein, King of Jordan.

On Saturday, 5 April the Holy Father received in audience:

– Cardinal Marc Ouellet, P.S.S., prefect of the Congregation for Bishops.

– Eight prelates of the Tanzania Episcopal Conference, on their “ad limina” visit:

– Bishop Tarcisius Ngalalekumtwa of Iringa, apostolic administrator “sede vacante ed at nutum Sanctae Sedis” of Songea;

– Bishop Bruno Pius Ngonyani of Lindi;

– Bishop Evaristo Marc Chengula, I.M.C., of Mbeya;

– Bishop John Chrisostom Ndimbo of Mbinga, with Bishop emeritus Emanuel A. Mapunda;

– Bishop Gabriel Mmole of Mtwara;

– Bishop Alfred Leonhard Maluma of Njombe;

– Bishop Castor Paul Msemwa of Tunduru-Masasi.

Papa atoa ujumbe kwa Maaskofu wa Tanzania

Katika mkutano wa hivi punde (ad limina)  na maaskofu toka Tanzania, Papa Francis ametoa ujumbe maalumu kwa  Maaskofu na Kanisa la Tanzania kwa ujumla.

TO THE BISHOPS OF TANZANIA: YOUR EXAMPLE INSPIRES THOSE WHO LONG FOR PEACE

Vatican City, 7 April 2014 (VIS) – This morning Pope Francis received in audience the bishops of the Tanzania Episcopal Conference, at the end of their five-yearly “ad limina” visit and, in the written address that he handed to them, he praises “the impressive history of missionary work throughout the region”, encouraging the prelates to “maintain and foster this missionary imperative, so that the Gospel may increasingly permeate every work of the apostolate and shed its light on all areas of Tanzanian society”.

“The work of evangelisation in Tanzania, then, is not merely a remarkable event of the past”, he writes; “no, it happens every day in the Church’s pastoral work in parishes, in the liturgy, in the reception of the sacraments, the educational apostolate, health care initiatives, catechesis, and in the lives of ordinary Christians”. The Pope mentions in particular the witness of healthcare workers who “care for those suffering from HIV/AIDS, and by all who strive diligently to educate people in the area of sexual responsibility and chastity”, and “all those who devote themselves to the integral development of the poor, and in particular, of destitute women and children”. He exclaims, “May the Holy Spirit who gave strength, wisdom and holiness to the first missionaries in Tanzania continue to inspire the entire local Church in this vital witness”.

He also repeats the importance of “holy, well-educated and zealous priests” and of ensuring they “receive an adequate human, spiritual, intellectual and pastoral formation”. With reference to the role of the laity, he asks that bishops make special efforts to “provide catechists with a comprehensive understanding of the Church’s doctrine. This will equip them not only to counter the challenges of superstition, aggressive sects and secularism, but even more importantly,to share the beauty and richness of the Catholic faith with others, particularly the young”.

With regard to the theme of the family, Pope Francis affirms that “The gift that healthy families represent is felt with particular vitality in Africa” and recalls that “the Church’s love for, and pastoral solicitude towards the family is at the heart of the new evangelisation. … By promoting prayer, marital fidelity, monogamy, purity and humble service to one another within families, the Church continues to make an invaluable contribution to the social welfare of Tanzania, one which, coupled with her educational and healthcare apostolates, will surely foster greater stability and progress in your country. There is scarcely a finer service which the Church can offer than to give witness to our conviction of the sanctity of God’s gift of life and to the essential role played by spiritual and stable families in preparing the younger generations to live virtuous lives and to face the challenges of the future with wisdom, courage and generosity”.

He concludes, “I am particularly encouraged to know that Tanzania is committed to ensuring the freedom that followers of various religions enjoy to practice their faith. The ongoing protection and promotion of this fundamental human right strengthens society by enabling believers, in fidelity to the dictates of their conscience and in respect for the dignity and rights of all, to advance social unity, peace and the common good. I am grateful for your ongoing efforts to promote forgiveness, peace and dialogue as you shepherd your people in difficult situations of intolerance and, at times, of violence and persecution. … I urge you also to work with government and civic institutions in this area so as to ensure that the rule of law prevails as an indispensable means for guaranteeing just and pacific social relations. I pray that your example, and that of the entire Church in your country, will continue to inspire all people of good will who long for peace”.

Papa akutana na Maaskofu wa Tanzania

Hivi karibuni maaskofu toka Tanzania walimtembelea Baba Mtakatifu katika matembezi yao ya kawaida ya kila baada ya miaka mitano ; Ad limina.

Kwa bahati nzuri, Wazo Huru imepata sehemu ya kilichotokea huko.

Unaweza kupata zaidi kwa kugonga kwenye muunganisho huo (kuondoa matangazo gonga neno skip Ad) :

 

 

Pd. Deogratias Mwansele Aliyetutoka

Hivi punde zimeanza kusambaa taarifa rasmi kuwa Pd. Deogratias Mwansele amefariki dunia leo saa kumi alfajiri katika hospitali ya jimbo Igogwe huko jimboni Mbeya alikokuwa akitibiwa kwa siku zake za mwisho.

Pd. Deo Mwansele akiwa na mbwa wake ampendae jimboni Mbeya

Pd. Deo Mwansele akiwa na mbwa wake ampendae jimboni Mbeya

Kwa mujibu wa taarifa za hivi punde. Padre Mwansele atazikwa Ijumaa saa nne asubuhi katika makaburi ya mapadre, Mwanjelwa, Mbeya.

Mmoja kati ya waleta ujumbe akitaarifu hilo tukio  aliandika “Kwa masikitiko napenda kukutaarifu kuwa kaka yetu Padre Atupele Deogratias  Mwansele amefariki leo  saa 10.00 alfajiri.”

Binafsi najikuta kuguswa zaidi kwa vile nilisaidiana naye kwa  ukaribu sana  kwa hili na lile. Alikuwa msaada mkubwa sana kwangu pia.

Nilipoongea naye siku chache zilizopita akiwa katika sauti yake ile ile nzito nzito alidai kuwa hali ilikuwa inatia moyo baada ya mahangaiko fulani fulani kiafya. Alionesha kuwa na uhakika wa kurudi  jimboni kuendelea na majukumu yake lakini mipango ya Mungu haikuwa hivyo.

Pd. Mwansele ambaye kwa wengi alijulikana kama “Padre Mpendwa” atakumbukwa na wengi kwa matani na vichekesho vyake katika mazingira mbalimbali.

Mbwa akitabasamu katika pozi la pamoja na Pd. Mpendwa, Deo Mwansele aliyetutoka

Mbwa akitabasamu katika pozi la pamoja na Pd. Mpendwa, Deo Mwansele aliyetutoka

Ni kutokana na  ucheshi wake  alitokea kumwita kila aliyekutana naye , “Mpendwa” ambapo nao walimwita “Padre Mpendwa”

“Hakika tutaikosa michapo mingi toka kwa Pd. Mwansele” alisema mmoja kati ya ya watoa huzuni zao.

Moyo wake wa kujituma katika kazi mbalimbali za kitume ulijidhihirisha zaidi alipohamishiwa pale Mbeya mjini kuwa paroko msaidizi kwa miaka hii ya karibuni hadi hatima ya maisha yake.

Hakika kanisa la Mbeya limeondokewa na mmoja kati ya nguzo muhimu katika uinjilishaji.

Mungu aipumzishe pema roho yake. Amina.

Re-incarnation : Je wafu hurudi na kuzaliwa upya?

Kuna wakati  ambapo matukio fulani katika maisha ya mwanadamu huibua maswali mengi. Moja kati ya suala hilo ni juu ya uwezekano wa baadhi ya wafu kuzaliwa upya.

Je, hilo lawezekana?  Hebu tutuatilie visa hivi . Pengine tunaweza kujikuta tumefahamu mengine mapya. Moja ya matukio hayo ni hili linahusu familia ya mtoto James Huston (au James 3). Je, umewahi sikia hilo?

Gonga katika sehemu hizo hapo:

http://www.youtube.com/watch?v=Uk7biSOzr1k

Na hapo pia:

http://www.youtube.com/watch?v=QgOBfCrxS3U

Suala la Transgender lachukua sura mpya : kubadili majina

Hakika tunamshukuru Mola kwa kutuvusha hadi huu mwaka mpya. Nianze kwa kumtakia matashi mema kila msomaji wa Wazo huru . Aidha, heri na fanaka kwa mwaka mpya , 2014.

Baada ya hayo napenda kukukushirikisha hili suala la akina Transgender (WAVUKAJINSIA kwa Kiswahili chepesi );  mtu ambaye ni wa jinsia ya kike ama ya kiume lakini akili yake ina msadikisha kuwa yeye ni wa jinsia tofauti na anavyoonekana kimaumbile.

Kwa mantiki hii japo huyo mtu anaweza kuonekana kuwa ni mwanaume kimaumbile lakini yeye kichwani mwake anajiona kuwa si mwanaume bali ni mwanamke. Hali hiyo hiyo hutokea hata kwa akina mama.

Hivi sasa watu wa mtindo huo hujulikana kwa kiingereza kama TRANSGENDER. Bado sina hakika juu ya Kiswahili chake (pengine ni WAVUKAJINSIA). Basi haidhuru hebu tuendelee.

Hivi punde hawa ndugu WAVUKAJINSIA wameamua kufanya kitu kingine kipya kwa kutafuta namna nzuri ya kubadili majina yao ili yaendane na jinsia wanazojisikia na si wanavyoonekana ili kurahisisha upatikanaji wa haki zao katika jamii.

Moja kati ya madai ya WAVUKAJINSIA ni kwamba nyakati zingine wamekuwa wakifedheheshwa na kutoeleweka pindi wanapojitokeza kufuatilia kazi zinazoendana na jinsia wanazoziamini kuwa nazo . Wanakutana na watu wasiowaelewa vizuri na kudhani wamechanganyikiwa.

Mfano mmoja wapo ni pale wanapokuta kazi zinatangazwa kwa ajili ya wanawake nao wanaenda kuomba kazi hizo (ingawa kimaumbile wanaonekana wanaume lakini wao wanaamini ni wanawake na siyo vinginevyo)  lakini wanadhalilishwa kwa kuambiwa wanatania kwani wao si wanawake hata kama wanajisikia kuwa wanawake.

Jitihada inayoanzishwa na wana WAVUKAJINSIA ni kuamua kufanya kitu kimoja , nacho ni kubadili majina yao. Kama alikuwa John atachukua jina la Maria.

Je, ndugu msomaji una maoni gani hapo?

Kwa kujua zaidi hilo, hebu gonga na kuipitia hiyo link hapa chini:

http://www.post-gazette.com/local/city/2014/01/02/Legal-project-helps-transgender-people-get-a-name-change-Transgender-people-get-legal-aid-to-alter-names/stories/201401020105